Translator's note on Kiswahili: Kiswahili is a Bantu language originally spoken by the Swahili people, who are found primarily in Tanzania, Kenya and Mozambique. (Read more about this translation over at the Appendix)

The death of children – Kiswahili

Kifo cha Watoto 

 

Ni kifo cha watoto kinachochukiza zaidi 

asili na haki. Hakuna haja kuuliza kwani. 

Haki ni nini, hakuna aelewaye. 

 

Ni adhabu ipi hurekebisha? 

Hakuna kisingizio, udhuru au pazia. 

Ni kifo cha watoto kinahochukiza zaidi. 

 

Yeyote anayepinga hujifanya 

kusoma mistari ya hatima. Lakini tuape kwa 

haki ni nini, hakuna aelewaye. 

 

Namna majaliwa au bahati hujisuka. 

Ateteaye malengo yao na sababu nzuri husema uongo. 

Ni kifo cha watoto kinachochukiza zaidi. 

 

Kifo hakistahili kuvuna faida kama hizo 

kutokana kwa hawa, ambao hawakuishi,  wazazi wao hulia. 

Haki ni nini, hakuna aelewaye. 

 

Leteni faraja basi, na kutia shime.  Wageni, marafiki 

sisi sote si wazazi watoto wanapokufa? 

Haki ni nini, hakuna aelewaye. 

Ni kifo cha watoto kinachochukiza zaidi. 

 

Translated by

Jane Bosibori Marando Obuchi

Featured in
Richard Berengarten’s ‘The Death of Children’
See the collection

Jane Bosibori Marando Obuchi

Jane Bosibori Marando Obuchi (b.1970) is a prolific and versatile writer, translator, researcher, scholar, teacher, educator, and singer and musician. (Read more about this translator over at the Appendix)

Photography credit: Ceejays Photography Eldoret.

Close